Psalms 89:39-44


39 aUmelikana agano lako na mtumishi wako,
na umeinajisi taji yake mavumbini.

40 bUmebomoa kuta zake zote,
na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu.

41 cWote wapitao karibu wamemnyang’anya mali zake;
amekuwa dharau kwa jirani zake.

42 dUmeutukuza mkono wa kuume wa adui zake,
umewafanya watesi wake wote washangilie.

43 eUmegeuza makali ya upanga wake,
na hukumpa msaada katika vita.

44 Umeikomesha fahari yake,
na kukiangusha kiti chake cha enzi.
Copyright information for SwhKC